Thursday, 27 March 2014

MAFIKIZOLO{SA}NDANI YA BONGO-APRIL 2014.

Kundi maarufu  la Muziki kutoka Afrika Kusini, Mafikizolo linatarajiwa kudondosha burudani ya aina
yake itakayoacha gumzo Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Mlimani City tarehe 5 mwezi Aprili mwaka huu, kwa ajili ya kuwapa burudani ya moja kwa moja wapenzi wa muziki wao hapa Tanzania.


Mafikizolo ambayo inaundwa na wakali Theo Kgosinkwe na Nhlanhla Nciza tayari wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kulishambulia jukwaa katika onyesho ambalo linakuwa ni la kwanza kabisa kulifanya hapa Bongo katika historia ya kundi hili.
Tiketi za onyesho hili linalosubiriwa kwa hamu, zitapatikana kwa shilingi 20,000 tu kabla ya show katika maeneo tofauti yatakayotangazwa hivi karibuni na mlangoni siku ya tukio zitapatikana kwa shilingi 35,000 tu.

No comments: