Friday, 14 March 2014

MAISHA KENYA YAPANDA KWA KIASI KIKUBWA.

Utafiti mpya nchini Kenya umeonyesha kuwa idadi kubwa ya wakenya wanakerwa zaidi na hali ya mfumuko wa bei na gharama ya juu ya maisha kuliko kitu kingine chochote.
Wasiwasi unaokuja baada ua mfumuko huo wa bei ni ukosefu wa ajira. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya utafiti kuhusu maswala ya kijamii na kisiasa IPSOS Synovate

Ripoti hii inakuja huku hoja ya kupunguza gharama ya matumizi ya serikali ikitawala vinywa vya wengi nchini humo.
Baadhi wanaona kuwa hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 haitazaa matunda kwani bado kuna changamoto ya ufisadi na uharibifu wa pesa za serikali.
o
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 81 ya waliohojiwa walisema kuwa wanategemea huduma ya matibabu katika hospitali za umma ambazo zinakabiliwa na changamoto za vifaa pia.
SOURCE-BBC SWAHILI.

No comments: