Thursday, 12 June 2014

UTEUZI WA NAIBU MABALOZI.

Bw. Robert Kahendaguza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Naibu Mabalozi wawili.
Walioteuliwa ni Bw. Robert Kahendaguza  anayekuwa Naibu Balozi, Ubalozi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, na Bw. Msafiri Marwa  anayekuwa Naibu Balozi wa Tanzania London, Uingereza.
Bw. Msafiri Marwa
 
Kabla ya uteuzi huu, Bw. Kahendaguza alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Marwa alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.
Uteuzi huu unaanza tarehe 25 Mei, 2014.
IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
JUNI 11, 2014

No comments: