Sunday, 16 March 2014

Mh,Mbunge Rose Kamili {CHADEMA}akamatwa na Polisi akigawa Rushwa Jimboni Kalenga!

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo{Chadema} amekamatwa leo na Polisi katika Kata ya Luhota kijiji cha Kitawaya akigawa pesa (rushwa) kwa wapiga kura wa jimbo la Kalenga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili, ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.
Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini kwa tuhuma za kugawa Fedha kwa wanakijiji hao, akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
 Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.

No comments: