Thursday, 27 March 2014

WASICHANA WAKITANZANIA WASHIRIKI BIASHARA YA UKAHABA{CHINA}

Serikali ya Tanzania imesema kuwa imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda nchini China kwa lengo la kuwashirikisha katika biashara ya ukahaba ambao unadaiwa kusababisha kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatifa nchini Tanzania Bw,Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina ambaye inasadikiwa alikuwa nchini humo akishiriki biashara hiyo ya Ukahaba.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya wahusika wa biashara hiyo ni Watanzania wenyewe wanaowasafirisha wasichana hao wadogo kwa kisingizio cha kuwatafutia ajira. Baadhi ya wanaosafirishwa hujikuta pabaya baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za kusafiria na kulazimishwa kushiriki biashara hiyo ya ukahaba.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es laam wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka serikali ichukue hatua.

No comments: