Mtoto aliyejeruhiwa na risasi
iliyomuua mama yake katika shambulio lililofanywa kwenye kanisa la JOY
OF JESUS Lililoko mjini Mombasa Nchini Kenya tukio lililotokea siku ya jumapili, amefikishwa jijini Nairobi
kwa Ndege tayari kwa upasuaji.
Satrin Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu
anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa katika Hospitali kuu ya
Kitaifa ya Kenyatta ili kuondoa risasi hiyo iliyoingia kwenye ubongo wake
baada ya kumuua mama yake aliyekuwa amembeba wakati wa shambulio hilo.SOURCE:-BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment