Wednesday, 30 April 2014

NDOA YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN KUFUNGWA MARA TATU.

Zikiwa zimebaki siku chache kabla wazazi wa North West hawajaungana na kuwa mwili mmoja, imefahamika kuwa mastaa hao Kanye West na Kim Kardashian watalazimika kufunga ndoa mara tatu.
Mtandao wa Radar Online umeripoti exclusive kuwa ndoa ya wawili hao inatarajiwa kuwa na hatua mbili kabla ya ile ya mwisho itakayofanyika Jijini Paris, Ufaransa mwishoni mwa mwezi ujao.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kinadai kuwa, ndoa ya kwanza ya Kim na Kanye itafungwa Kusini mwa California huku ya Ndoa ya pili na ya tatu zitafungwa Ufaransa.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa mwanasheria wa wachumba hao amewashauri waanze kwa kufunga ndoa ya kiserikali nchini `Marekani, kabla ya ile kubwa ya Ufaransa ya May 24 ili kuepukana na vikwazo vya kisheria.
“Typically, the U.S. recognizes citizens getting married in France, but dealing with a foreign government and paperwork could be a nightmare,” Chanzo hicho kilisema. “So just to make sure it’s legal, Kim and Kanye will first be having a civil ceremony in Southern California.”
Baada ya hapo ndipo wapenzi hao wataelekea jijini Paris, ambako nako sheria ya Ufaransa inahitaji wanandoa kuwa na sherehe mbili za ndoa. Yaani Kabla ya ndoa ya kanisani kufungwa, cheti cha ndoa ya kiserikali huhitajika pia.
“A religious ceremony has to be performed after a civil ceremony, never before,” Ubalozi wa Ufaransa ulioko Washington D.C ulliambia Radar Online kama uthibitisho juu ya hilo.

No comments: