Juhudi za kukuza uchumi Afrika Mashariki hazitafanikiwa iwapo rushwa haitadhibitiwa-Dk.Reginald Mengi
Mwenyekiti
wa mfuko wa sekta binafsi nchini Dk. Regnald mengi amesema
itakuwa vigumu kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukuza uchumi
kama hazitadhibiti tatizo sugu la rushwa linaloendelea kujikita katika
sekta mbalimbali
Dr.Mengi
ameyasema hayo jijini arusha katika hafla ya utiaji saini mkataba wa
msaada wa euro milioni 2.3 zilizotolewa na jumuiya ya ulaya kwa ajili
ya kuimarisha ulinzi katika ukanda wa bahari ya hindi.
Dk.Mengi
ambaye pia ni mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya ipp amesema tatizo
la rushwa limeendelea kushika kasi na udhibiti wake unaendelea kuwa
mgumu kutokana na utaratibu unaotumika kulishughulikia ambao umejikita
zaidi kwa wanaotoa kwa watu wadogo.
Kwa
upande wake mwenekiti wa baraza la wafanyabiashara afrika
mashariki Bw. Felexs Mosha na mwenyekiti wa watendaji wakuu wa
makampuni nchini bw ally mafuruku wamesema pia nchi za
wanachama wa jumuiya hiyo zinakabiliwa na tatizo la gharama
kubwa za uwekezaji na ukosefu wa taarifa muhimu
Naye
naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia
fedha na utawala Jean Cloude amesema msaada huo wa jumuiya ya
ulaya utasaidia kuimarisha ulinzi hasa eneo la bahari ya hindi .
Balozi
wa umoja wa Ulaya hapa nchini Bw.Filiberto Sebregondi pamoja na
kuelezea azma ya jumuiya ya ulaya ya kuendelea kuisadia
jumuiya ya afrika mashariki amesema pamoja na changamoto
zinazojitokeza zikishughulikiwa upo uwezekano mkubwa wa
kufikiwa kwa malengo tarajiwa
Msaada
huo wa euro milioni 2.3 kutoka jumuiya ya ulaya (eu) ni
mwendelezo wa kampeni za jumuiya hiyo kuisadia jumuiya ya
afrika mashariki ,ambapo kwa kipindi cha mwaka 2010 kiasi
cha euro mili 37.5 zimetolewa
No comments:
Post a Comment