Tuesday, 20 May 2014

JB ADONDOKA AKIMUELEZEA MAREHEMU KUAMBIANA LEADERS

Msanii Jacob Steven ‘JB’ amedondoka katika Viwanja vya Leaders wakati akimuelezea msanii mwenzake marehemu Adam Kuambiana. 
Tukio hilo limetokea wakati wa zoezi la kuaga mwili wa marehemu kabla ya maziko yatakayofanyika baadaye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Marehemu Kuambiana alifariki dunia ghafla Jumamosi ya Mei 17 mwaka huu wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar.


Star huyo mkubwa wa filamu nchini Jacob Stephen(JB) ambaye hivi majuzi alienda nchini Uturuki kwa ajili ya ziara ya kikazi kwa wiki mbili amekatisha ziara yake hiyo na kurudi nchini kuja kumzika msanii mwenzake Adam Kuambiana aliyefariki juzi. JB tayari alishafanya kazi kadhaa na Kuambiana kwani hata filamu yake mpya iliyotoka wiki kadhaa nyuma inayoitwa Hukumu Ya Ndoa Yangu imeongozwa na Adam Kuambiana. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii jana JB aliandika "Tumefanikiwa kupata nafasi moja tu ya kurudi Dar es salaam kwa ajili ya msiba .ahsanteni wenzangu kwa kukubali niwawakilishe, mbaki salama nawapenda.". Kuambiana anazikwa leo Jumanne . Katika safari ya Uturuki ambayo imedhaminiwa na Princess Casino JB aliongozana na Wasanii wenzake Ray, Irene Uwoya na King Majuto.

No comments: