Friday, 2 May 2014

KUMBUKUMBU YA SIKU YA KUZALIWA SOPRANO YAAMBATANA NA BARAKA YA KUPATA MTOTO.

Leo ni siku ya kuzaliwa mkali wa Muziki wa RnB{Bongo},Soprano a.k.a Soprano Music,kikubwa kati ya yote kilichoifanya ilete utofauti siku hii ya kuzaliwa msanii huyu mkali{Bongo}ni baraka ya kupata mtoto wake wa kiume na wa kwanza katika siku ya jana,Soprano ameielezea furaha yake hiyo kwa mashabiki wake akifumbua siri nyingine kuwa hata katika mwezi huu huu pia mama wa mwanae pia ndiyo mwezi aliozaliwa,hivyo kufanya kuwa mwezi huu wa tano kwao kuwa ni mwezi wa kihistoria maishani mwao,kwa kusherehekea kumbukumbu za kuzaliwa wao wote watatu,baba,mama na mtoto. huu ndiyo ujumbe alioshiriki Soprano na mashabiki wake,
"Namshukuru MUNGU jana tarehe 1 amezaliwa mtoto wangu wa kwanza my baby boy ''JADEN CRUZ'' na siku km ya leo tarehe 2 ya mwezi km huu baba ake pia alizaliwa na tarehe 5 mwezi km huu Mama ake Alizaliwa pia tunafuraha sababu baba mama na mtoto wote tumezaliwa mwezi mmoja ila leo ni birthday yangu jaman nna furaha ambayo cwezi kuielezea."





No comments: