Thursday, 8 May 2014

MASTER JAY ASHANGAZWA NA DIAMOND KUPATA TUZO SABA WAKATI PRODUCER ALIYETENGEZA KAZI HUSIKA KUTOKA PATUPU.

Baada ya tuzo za KTMA kumalizika kila mmoja amekuwa na mtazamo wake, wiki hii producer wa wimbo wa ‘Number One’ wa Diamond, Sheddy Clever alitoa malalamiko yake ya kukosa tuzo ya mtayarishaji bora huku wimbo alioutengeneza ukimpa Diamond zaidi ya tuzo tano.Producer mkongwe Joachim Kimaryo aka Master J ametoa mtazamo wake kuhusu tuzo za KTMA 2014 ambao unaonesha hakuridhishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa mwaka – kizazi kipya ambaye ni Man Water wa Combinenga.
“Sijaelewa damond kupata tuzo 7 alafu produza wake kutoka na 0!!!!!” ni jibu la moja ya maswali kuhusiana na tuzo hizo aliyokutana nayo Master J Jana alipokuwa mgeni katika session ya ‘Kikaangoni Live’ kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.
Shabiki mwingine aliuliza: “Pia man water ni mkali au unasemaje master J?”
Na hiki ndicho alichojibu Jay: “mkali lakini hakustahili kushinda mwaka huu”

Swali tofauti na muziki ambalo lilijirudia mara nyingi ni kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake msanii Shaa, shabiki mmoja aliuliza:
“Mnafunga ndoa lini wewe na Shaa manaake mnapendezana kweli? Au ni mchepuko tu wa lami?

Na jibu la Joachim aka Master J lilikuwa kama ifuatavyo,mabibi na mabwana Ndoa yetu inakuja “SOON”.

No comments: