Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar
es slaaam. Habari zilizotua ndani ya Ngessa blogspot na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa
Bongo Movie, Bw,Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana
kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali
yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya
na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii
mwingine wa Bongo Movie Marehemu Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki
kimeleta mshituko mkubwa kwenye tasnia ya filamu za kibongo. Habari na
picha zaidi zitawajia baadae.
![]() |
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya taarifa za msiba wa msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' mapema leo. |
![]() |
Mume wa marehemu Recho, George Saguda,akiwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha mkewe. |
No comments:
Post a Comment