Mmoja kati ya waimbaji nyota wa muziki wa dansi waliowahi kutokea hapa nchini Amina Ngaluma amefariki dunia. Amina Ngaluma ni mmoja kati ya waanzilishi wa bendi za Tam Tam na Double M Sound,bendi zilizotamba sana mwanzoni mwa mwaka 2000 na kuendelea,Marehemu Amina Ngaluma amefia nchini Thailand alipokuwa akiishi kikazi kwa muda mrefu"Amina
Ngaluma 'Japanese' amefariki dunia akiwa nchini Thailand baada ya
kupatwa na uvimbe kichwani. Mpaka mauti yanamfika, Amina alikuwa
mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors. Msiba upo Kipunguni B, Machimbo
jijini Dar es Salaam." .Moja ya nyimbo zilizompa umaarufu sana enzi za uhai wake ni Mgumba No.1 aliouimba na bendi ya African Revolution 'Tam Tam' chini ya Mwinjuma Muumin.
Tungependa kuwapa pole ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa familia,mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen. -

No comments:
Post a Comment