Thursday, 5 June 2014

MAHAKAMA YATOA HUKUMU JUU YA NANI MMILIKI SAHIHI WA NYIMBO ZA MAREHEMU BOB MARLEY.

Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za Mfalme wa Muziki reggae duniani umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wake.
Jaji katika mahakama kuu jijini London{Uk}, Richard Meade ameifuta kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.

Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.

No comments: