Watumiaji wa mitandao ya kijamii juzi walishitushwa na picha zilizosambaa
mitandaoni zikimuonesha mhe. Captain John Komba (MB) akiwa faragha na msichana.
Mh Komba ambaye yuko Dodoma kwa ajili ya kikao cha bunge la bajeji amezungumza kuhusu picha hizo na kueleza kuwa hafahamu hata mazingira yanayoonekana katika picha hizo na kwamba picha hizo zimemuogopesha sana.
“Picha nimewahi kupiga nyingi sana tangu niko utotoni lakini hizi za leo hata mimi zinaniogopesha.”
Ameongeza kuwa hamfahamu mtu aliyesambaza picha hizo japo anajua lazima ni adui yake katika nyanja yoyote na akagusia pia madhara aliyoyapata kutokana na picha hizo kusambaa.
“Siwezi kuwa mwaguzi kusema nani amefanya hivyo lakini ukiangalia kuna roho ya uadui kati yangu mimi na huyo mtu ambaye ameamua kunifanyizia. Ameamua kuingia vitani, na anaweza kufanya hivyo kwa namna nyingi inaweza kuwa kisiasa au kirafiki lakini zimenipa tabu sana, zimeisumbua familia yangu na marafiki zangu. Kwa kweli zimenisumbua sana.”
Ameeleza kuwa katika picha hiyo mwili uliowekwa sio wake lakini umeunganishwa na kichwa chake na kwamba kama kweli picha hizo zingekuwa za kwake basi angeonekana na yeye akiwa mtupu kwa kuwa binti aliye kwenye picha hizo anaonekana kwenye picha nyingine akiwa mtupu.
Amesema familia yake imempigia simu na kumpa pole pamoja na marafiki zake japo wachache walipiga na kumtolea lugha chafu. Komba ameitaka jamii kumuogopa Mungu.
“Nikijua aliyenifanyia hivyo, akija kuniomba msamaha nitamsamehe lakini hili suala limeniathiri sana kisaikolojia hata bungeni leo sijaenda.”

No comments:
Post a Comment