Thursday, 12 June 2014

MTOTO WA KIKE WA R.KELLY AJITANGAZA KUBADILI JINSIA NA KUWA MVULANA (TRANSGENDER)

Mtoto wa kike wa mfalme wa R&B Robert Kelly aka R.Kelly mwenye miaka 14 amejitokeza hadharani na kujitangaza kuwa anataka kubadilisha jinsia na kuwa mvulana.
Mtoto huyo aitwaye Jaya ametangaza maamuzi yake hayo kwa dunia kupitia mitandao ya kijamii.
Jaya aliyezaliwa na jinsia ya kike amesema hivi sasa anajihesabu kuwa ni mvulana na kutangaza rasmi jina lake jipya {Jay}.
Jay amesema kuwa pamoja na mama yake mzazi aitwaye Andrea Kelly kumsupport kwa uamuzi aliouchukua, baba yake R.Kelly bado hajasema chochote juu ya hilo.

 "My mom was like, ‘Baby, you know I love you if you were bi, gay, lesbian, you name it and I would still love you so much’,” aliandika Jay katika profile yake ya Ask.fm. “I believe I am a boy and want surgery, and the medication to help me (be) who I was supposed to be.”
Jay amesema alijigundua kuanza kuvutiwa na wasichana akiwa na miaka 6, lakini ameongeza kuwa bado hahitaji kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa sasa.  

No comments: