| FLORA MBASHA |
![]() |
| SEHEMU YA CHUMBA CHA KUPUMZIKIA KILICHOACHWA KOCHI DOGO NA ZULIA PEKEE. |
Kwa mujibu wa mtu aliyeambatana na Mbasha alipopata dhamana dhidi ya kesi yake inayomkabili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, alipofika nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar alipigwa butwaa kukuta hakuna vitu ndani!
![]() |
| SEHEMU YA CHUMBA KINGINE KILICHOKOMBWA KILA KITU |
Ilielezwa kuwa vitu hivyo vilihamishwa Juni 16 ambapo Mbasha alitoka mahabusu Juni 17, yaani siku moja tu.
KITANDA CHA BEI MBAYA
Baadhi ya vitu vilivyodaiwa kuchukuliwa nyumbani hapo ni kitanda cha bei mbaya walichokuwa wakilalia kwenye chumba cha baba na mama huku akimwachia neti ikiwa inaning’inia.
SUTI ZA MAREKANI
Vingine ni makochi huku akibakisha sofa ndogo ya mtu mmoja, vitu vyote jikoni na nguo (suti za bei mbaya, walizonunua wakati wakiwa Marekani).
Pia alidaiwa kukomba vile vidani vyote vya dhahabu.
![]() |
| Mwanahabari akimhoji Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha Mzee Maneno. |
Ukiacha zile hati za nyumba, viwanja na mashamba, gharama ya vitu vyote vilivyochukuliwa ndani ni zaidi ya Sh. milioni 13 za Kitanzania (kama zile ambazo Wema Isaac Sepetu alizomlipia Kajala Masanja asiende jela).
AMWAGA CHOZI
Baada ya kukutana na mazingira ya aina hiyo, lilikuwa ni pigo lingine zito kwa Mbasha ambaye alijikuta akimwaga chozi kwa mara nyingine kwa sababu ya mkewe Flora aliyedumu naye katika ndoa kwa takriban miaka 12.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha aliumia kupita kiasi huku akiomba Watanzania waone ubaya aliotendewa.
![]() |
| Mwanahabari akimhoji Mama Mzazi wa Emmanuel Mbasha |
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Amani lilifika nyumbani hapo ambapo lilipata mwanya wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kisha kupekuwa chumba hadi chumba na kujionea kulivyokuwa kweupe huku madirishani mapazia yakiendelea kubembea kwa upepo mkali uliopo Dar kwa sasa.
Kimuonekano, nyumba hiyo ilikuwa kama kuna familia ilihama hivyo inahitaji kupangishwa au kuhamiwa na mwingine.
![]() |
| Emmanuel Mbasha |
Alipotafutwa Mbasha kuzungumzia ishu hiyo alikiri kukuta hali hiyo nyumbani kwake baada ya kupata dhamana.
“Nilipofika nyumbani kwangu nilikuta ufunguo wa nyumba kwa majirani. Niliwauliza kama kulikuwa na mtu anaingia nyumbani nikaambiwa ni Flora. Kama mnavyoona kuna vitu vingi vya ndani havipo,” alisema Mbasha.
Alipoulizwa kama ana uhakika kuwa mhusika ni Flora, Mbasha alisema yeye alikuta nyumba nyeupe.
Jitihada za kumpata Flora hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani haikuwa hewani juzi Jumanne mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya Mbasha kukabiliwa na kesi hiyo ya madai ya ubakaji wa ndugu wa Flora, Mei 23 na 25, mwaka huu, tayari kulikuwa na mgogoro wa ndoa. Flora alishaondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza jijini Dar.
ANGALIA VIDEO IKIMUONYESHA EMMANUEL MBASHA{MUME}WA FLORA MBASHA AKIFUNGUKA JUU YA HILO,






No comments:
Post a Comment