Wednesday, 23 July 2014

Cristiano Ronaldo ajiingiza kwenye mitindo, aanzisha nembo yake ya viatu

Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezidua nembo yake rasmi itakayotumika kwenye viatu maaalum.
Kwa mujibu wa Mirror, mchezaji huyo amefuata nyayo za wachezaji wengi wakubwa waliowahi kuanzisha brand zenye majina yao katika mitindo.
Cristiano Ronaldo Footwear’ kama ilivyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook itatumika kwa viatu vinavyotengenezwa nchini Uholanzi peke yake.
Viatu hivyo vinatarajiwa kutengenezwa kwa kuzingatia utambulisho, taswira na tabia ya Cristiano Ronaldo.



No comments: