Beki na nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Brazil, David
Luiz Moreira Marinho, amewataka radhi mashabiki wa soka wa nchi hiyo
kufuatia kisago cha mabao saba kwa moja walichokipokea kutoka kwa
Ujerumani usiku wa kuamkia hii leo huko Estádio Mineirão, mjini Belo
Horizonte.
Luiz, ambaye alichukua jukumu la kukiongoza kikosi cha Brazil
kufuatia nahodha Thiago Silva, kutumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi mbili
za njano, amesema mpaka sasa hawajui nini kilichosababisha kupokea
kisago hicho ambacho kinaiingiza nchi hiyo katika rekodi mpya kwenye
medani ya soka duniani.
Amesema wanatambua mashabiki wa soka nchini humo, wameumizwa sana na
kichapo hicho, lakini akasisitiza hawana budi kusamehewa na kuendeleza
umoja waliokuwa nao kama walivyoanza fainali za kombe la dunia za mwaka
huu June 12.
Kwa upande wa mlinda mlango wa Brazil, Julio Cesar amesema soka lina
maajabu yake na usiku wa kuamkia hii leo, maajabu ya hatari yaliwageukia
wao kama wenyeji, hivyo hawana budi kukubaliana na hili hiyo.
Timu ya taifa ya Brazil imekubali kufungwa mabao saba kwa moja na
kuwa timu ya kwanza duniani kufungwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo
wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia.
Mabao ya Ujerumani katika mchezo huo yalipachikwa wavuni na Thomas
Müller, Miroslav Klose, Sami Khedira, Toni Kroos aliefunga mabao mawili
pamoja na André Horst Schürrle aliefunga mabao mawili pia.
|
No comments:
Post a Comment