Thursday, 17 July 2014

MGANGA ANASWA LIVE GUEST NA WAKE ZA WATU.

Mganga wa Jadi Bw,Wadebi Jinasa.
Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi akijutia baada ya kunaswa live.

Ama kweli uswazi hakuishi vijimambo! Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa amepata aibu ya karne baada ya kunaswa ‘live’ na wake za watu kwenye gesti moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam

Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.
Sangoma huyu amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea....

No comments: