Thursday, 24 July 2014

Watu sita wameuawa akiwemo mlinzi mmoja wa Rais Joseph Kabila

Watu sita wameuawa akiwemo mlinzi mmoja wa Rais Joseph Kabila na waasi 23 wanashikiliwa baada ya mapigano yaliyoibuka ghafla katikati ya jiji la Kinshasa huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kati ya jeshi la DRC na waasi kutoka Congo Brazaville ambao zamani walikuwa askari wa Mobutu Seseseko kabla ya kukimbia nchi hiyo.
Taarifa kutoka serikali ya DRC imesema imedhibiti hali ya mambo na msako unaendelea kutafuta waasi hao walioingia mjini wakiwa na silaha mchanganyiko.
Pia  Kumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zinasema kuwa raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika makabiliano hayo yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais yametokana na nini.

Wadadisi wa mambo wanahisi kwamba kisa hiki huenda kikazusha utata tena kati ya Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kwa vile shambulio lilitokea karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa kutoka kwa serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kujipenyeza katika kambi ya kijeshi ya Camp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya dakika 30 hivi.

Jamhuri hiyo ya Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na hata rais aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila alichukua mamlaka baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.

Duru zinasema kuwa wavamizi takriban 20 walijaribu kuingia ndani ya kambi hiyo lakini shambulizi likazimwa .
Raiya walihamishwa kutoka maeneo yaliyoko karibu na uwanja wa ndege ulifungwa wakati wa shambulizi hilo.
Serikali bado haijamtaja nani aliyeishambulia .

Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila walilaumiwa.

No comments: