Thursday, 14 August 2014

AFANDE SELE AFIWA NA MAMA WATOTO WAKE.

AFANDE SELE

Aliyekuwa mke wa Msanii Mkongwe Afande Sele (Waliachana baadae) aliyezaa nae watoto wawili (Tunda na Sanaa) amefariki majira ya sita usiku wa kumkia leo. Akiongea na tovuti ya Times Fm kupitia simu yake ya mkononi  msimamizi wa kazi za Afande Sele aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Busanda amesema kuwa mama Tunda alifariki kutokana na ugonjwa wa malaria uliomsumbua kwa muda wa siku tatu. “Alilazwa katika hospitali ya St. Mary Morogoro akatolewa jana lakini usiku hali yake kidogo ilizidi kuwa mbaya ndipo akapelekwa hospitali kubwa ya Morogoro na umauti ukamkuta hapo. Aliugua kwa muda wa kama siku tatu.” Jackson Busanda ameiambia tovuti ya Times Fm. Akizungumzia hali ya Afande Sele kwa sasa, amesema kuwa Afande Sele alizimia alipokuwa anaenda kuuona mwili wa marehemu. Kuhusu utaratibu wa mazishi,
AFANDE SELE,MKEWE NA WATOTO ENZI ZA NDOA YAO

 amesema kuwa familia imepanga kufanya mazishi leo majira ya saa tisa mchana katika makaburi ya Kola, mjini Morogoro. Marehemu ameacha watoto wawili ambao ni Tunda na Sanaa. Tunampa pole Afande Sele, tunamuombea apate nguvu ya kuvuka kipindi hiki kigumu. Mama Tunda apumzike kwa amani. Amina. Afande aliandika ujumbe kwenye Facebook na Instagram kutoa taarifa ya msiba huo.
***TAARIFA KWA SAUTI,

No comments: