Wanafunzi 28,037 watakosa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu hivyo watalazimika kusaka njia mbadala kama
wanataka kuendelea na masomo yao. Hadi kufikia julai 31 wanafunzi
58,037 walikuwa wametuma maombi ya mikopo na bodi hiyo imesema ina uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 tu.
Pia kuhusu madai ya wanafunzi wa vyuo vitano kutaka wapewe bilioni 6.6 kwaajili ya mafunzo ya vitendo, bodi ya mikopo imesema malipo hayo yataandaliwa na kwamba hundi za malipo hayo zinatarajiwa kupelekwa katika vyuo wiki ijayo.
Vyuo hivyo ambavyo havijapata fedha ni SAUT, IFM, Teofilo Kisanji- Mbeya, Tumaini, SMUCCO na Jordan cha Morogoro

No comments:
Post a Comment