Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaada mkubwa katika nyimbo zao zote. “Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies tu na yeye huwa anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno moja baada ya moja.” Amesema Asley. “Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.
RAHA MASTERS INC & GRAPHIC DESIGNERS. FIND US ON:-FACEBOOK as Ngessakinollo OR dvjKson on INSTAGRAM.
Saturday, 16 August 2014
Yamoto Band wamtaja anaewaandikia nyimbo kwa asilimia 90
Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaada mkubwa katika nyimbo zao zote. “Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies tu na yeye huwa anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno moja baada ya moja.” Amesema Asley. “Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment