Thursday, 11 September 2014

Mcheza mieleka wa zamani bingwa wa WWE ajiua kwa kujinyonga

Sean O'Haire

Mcheza mieleka wa zamani wa WCW na WWE, Sean O’Haire amekutwa akiwa amefariki baada ya kujinyonga, Jumanne wiki hii. Kwa mujibu wa jarida la TMZ, polisi wameeleza kuwa walimkuta O’Haire akiwa chumbani kwake South Carolina akiwa amejifunga kamba shingoni na tayari akiwa ameshakufa. Mwili wake ulitambuliwa kwa mara ya kwanza na baba yake mzazi ambaye aliwapigia simu polisi. O’Haire ambaye jina lake halisi na Sean Hair aliingia katika ulimwengu wa mieleka kwenye WCW (World Championship Wrestling) mwaka 2000 na mwaka huo alipewa ubingwa wa ‘Rookie of the Year’. Yeye na partner wake Chuck Palumbo waliwahi kuwa mabingwa wa WCW kabla ya kampuni hiyo kununuliwa na WWE. Mwanamieleka huyo alifahamika zaidi kwa utambulisho wa sentensi yake mara kwa mara “I’m not telling you anything you don’t already know.”

No comments: