![]() |
| Meninah |
YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi. akizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond. Chanzo hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
![]() |
| Wema Abraham Sepetu |
Ilisemekana kwamba baada ya Wema kuzinyaka habari hizo kuwa anataka kunyakuliwa ‘beibi’ wake mbaya zaidi wanataka kufunga ndoa, malkia huyo mkubwa wa sinema Bongo aligeuka mbogo na kuanza kuweka mikakati ya kumteketeza Meninah asiweze kufunga ndoa na Diamond.
Kuna madai kwamba Meninah aliposikia Wema anamsaka usiku na mchana ili amshikishe adabu, msanii huyo alishtuka kwa kuwa anaujua vizuri ‘mziki’ wa staa huyo.
VIKAO VYA HARUSI VYAFANYWA
Taarifa ziliendelea kudai kwamba, vikao vya harusi vya chinichini vinaendelea kufanywa huku wahudhuriaji wakiwa ni mdogo wa Diamond ambaye pia ni mwanamuziki, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darlin’ pamoja na baadhi ya ndugu wa upande wa mama Diamond ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa.
![]() |
| Diamond Platnumz |
POMBE NA STAREHE VYATAJWA
Sababu kubwa inayosemekana Wema kutemwa kuolewa na Diamond ni kutokana na kuendekeza pombe na starehe jambo ambalo Meninah yupo nalo kando na kwamba hivi sasa amekuwa akitimba kwa mama Diamond bila wasiwasi huku akizama jikoni kupika, kupakua na kufanya kazi ndogondogo za ndani ili kuthibitisha kuwa yeye ni mama bora.
DIAMOND AMTOA MACHOZI
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilimsaka Meninah na kumhoji juu ya sakata hilo la kutaka kuolewa na Diamond ambapo alikuwa na haya ya kusema:
| Meninah |



No comments:
Post a Comment