![]() |
| Lady Jay Dee{Anaconda} |
HABARI mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wawili hao walidaiwa kufikia uamuzi wa kuvunja mkataba baada ya kuona ndoa yao inasuasua kutokana na migogoro.“Lady Jaydee au Jide alipoona mambo yanakwenda ndivyosivyo alimshauri Gardner wavunje mkataba wa Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe na businesses (biashara) zake. “Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
![]() |
| Gadner.G.Habash & Lady Jay Dee. |
Source-GPL.


No comments:
Post a Comment