![]() |
| Vanessa Mdee{Vee Money} |
Akiwa anahojiwa na jarida moja la huko nchini Kenya Vanessa Mdee, afunguka mengi ambayo hajawahi kuyasema sehemu nyingine yeyote ile, na kwa wengi wanaomfahamu mkali huyu wa anayezidi ku-make headlines na single yake ya “hawajui”, watabaki midomo wazi kwa vile ambavyo walikuwa hawavijui kabisa kuhusu mwanamuziki huyu kutoka Tzee.
Moja ya mambo ambayo vanessa huwa hafanyi kabisa mbali na kuwa mwanamuziki, mtangazaji na mwanaharakati ni kupika, Vanessa alifunguka na kusema hata akiwa nyumbani kwake ishu nzima ya kupika haimjii akilini kabisa. Tofauti na wanawake wengi wa afrika, hii ishu ni moja kati ya vitu vilivyotokea kuwashangaza wapenzi wengi na wadau wanao mzimia Vanessa.
![]() |
| Vanessa Mdee |


No comments:
Post a Comment