Friday, 14 November 2014

KIONGOZI WA KANISA LA THE POOL OF SILOAM INTERNATIONAL MINISTRIES ATANGULIA MBELE YA HAKI.

Mtume na Nabii ELIYA.
KIONGOZI WA KANISA LA "THE POOL OF SILOAM CHURCH" LENYE MAKAO YAKE MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM,MAENEO YA MBEZI BEACH{MAKONDE},MTUME NA NABII ELIYA AMETANGULIA MBELE,
TAARIFA ZA AWALI ZILIZOTUFIKIA TOKA KWA MKE WA MTUMISHI HUYO WA MUNGU ZINADAI KUWA MTUME NA NABII ELIYA ALIFARIKI DUNIA JANA USIKU,
AKIELEZEA HILO MKEWE ANADAI MAREHEMU ALIKUWA BUHERI WA AFYA TOKEA MCHANA HADI KUFIKA MUDA WA USIKU ALIPOKUWA NAYE,AMBAPO KABLA YA UMAUTI KUMFIKA WALITAKIWA KUWEPO KWENYE HUDUMA YA MUNGU,AMBAPO BAADA YA KUMALIZA KUJIANDAA KWA SAFARI HIYO{MKEWE}ALISHANGAA KUMUONA MTUME AKIWA KATIKA HALI KANA KWAMBA HANA JUKUMU LINGINE KWA SIKU HIYO,KWANI HAKUWA KATIKA HALI YA KUJIANDAA KUTOKA TENA NYUMBANI,NDIPO ALIPOMUULIZA NA KUMJIBU "MKE WANGU MIMI KAZI ALIYONITUMA MUNGU NIMEKWISHA IMALIZA",KISHA MTUME ALILALA KWENYE KOCHI NA NDIPO UMAUTI ULIPOMFIKA PAPO HAPO,
TAARIFA HIZI ZIMEPOKELEWA TOFAUTI NA WAUMINI WA KANISA HILO,HUKU WENGI WAKIONYESHA KUFARIJIKA NA KIFO CHA MTUME WAO WAKISISITIZA KUWA KIFO HICHO KIMETHIBITISHA KUWA MTUME ELIYA ALIKUWA NI MTUMISHI WA MUNGU HASWA KWANI AMETANGULIA MBELE YA HAKI KWA KUNYAKULIWA KAMA BIBLIA INAVYOSEMA BILA KUCHANGAMANA NA MATESO YA DUNIA KABLA YA UMAUTI.
IKUMBUKWE MTUMISHI WA MUNGU NABII NA MTUME ELIYA NDIYE ALIYEPEWA MAONO JUU YA KALENDA SAHIHI YA KIUNGU,KALENDA INAYOONYESHA UTOFAUTI WA SIKU PAMOJA NA SIKUKUU ZOTE ZILIZOMO KWENYE KALENDA,
MAONO YALIYOPOKELEWA KWA MTAZAMO TOFAUTI NA WAKRISTO PAMOJA NA DINI NYINGINE TOFAUTI NCHINI TANZANIA ILI KUFUATILIA KWA UKARIBU KALENDA HIYO YA KIUNGU INGIA HAPA>>>http://www.siloamgoshen.org/
     TARATIBU ZA KUUPUMZISHA MWILI WA MAREHEMU ZINAENDELEA NYUMBANI KWA MAREHEMU..

No comments: