![]() |
Sitti Mtemvu siku aiyovishwa Taji la Redds Miss{TZ}2014. |
Barua ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu aliyowaandikia Lino International Agency kuhusu uamuzi wake wa kujivua taji hilo. Hatimaye kampuni ya Lino International Agency imemvua taji aliyekuwa mrembo wa Tanzania 2014 (Redd’s Miss Tanzania 2014) Sitti Abbas Mtemvu kwa kosa la kudanganya umri katika mashindano hayo.
![]() |
Barua ya Sitti Mtemvu yakujivua taji la Redds Miss{TZ}2014. |
Baada ya kukabidhiwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2014 Oktoba 11, siku chache baadae Sitti alikumbwa na kashfa ya kudanganya umri baada ya kuonekana kuna utofauti wa umri kati ya leseni na pasipoti yake. Taji hilo litakabidhiwa kwa mshindi wa pili Lilian Kamazima.
No comments:
Post a Comment