 |
| Paul Makonda |
Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionyesha kwenye simu yake picha ya video iliyopigwa wakati wa vurugu zilizotokea wakati wa mdahalo wa kujadili rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza juzi, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo.
 |
| Paul Makonda |
Makonda akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi kubwa aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Jaji Warioba kutoka salama pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho ambaye pia alikuwa anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.
 |
| Paul Makonda mbele ya wanahabari. |
Makonda akiendelea kuelezea kuwa anasikitishwa na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii iliyomzulia kwamba yeye ndiye aliyesababisha vurugu wakati siyo. Pia amelaani watu wote waliosababisha vurugu hizo kwamba kitendo hizho kinadhoofisha demokrasia nchini.
No comments:
Post a Comment