Wednesday, 19 November 2014

Post Ya Diamond Kuhusu Meda, Msanii Aliyeimba Wimbo Wa Barua Kwa Diamond

Kwenye Exclusive interview na Meda Msami, alifunguka kuwa anamkubali vilivyo Diamond na kwamba huko kwao Iringa yeye ndiye balozi wa Diamond, alipitia tabu sana kumtafuta miaka miwili iliyopita na sasa ameamua kufanya wimbo huu kama zawadi kwake na pia kuonyesha anavyo mkubali
Hii hapa ni post ya Diamond kuhusu kazi ya Meda.
"Kiukweli simfahamu... Sijawai hata kumuona, Wala kuzungumza nae.....na sio kwasababu Eti kaniimba mimi, hapana!... ila ni Userious na uzuri wa kazi aliyoifanya ndio vimenifanya nione ni vizuri kumleta kwenu hapa wadau ili kwa pamoja tumsupport naye kesho na keshokutwa afikie malengo ya kazi yake na kuwa Balozi mzuri wa nchi yetu kupitia Bongo flavour..Huyu hapa! anaitwa MEDA kutoka IRINGA"
  

Meda - Barua kwa Diamond [Official Music Video]

No comments: