Friday, 23 January 2015

KUNA TATIZO KWANI?

Diamond Platnumz & Mh,Rais Jakaya.M.Kikwete.

DIAMOND PLATINUMZ, RAIS JK SIRI NZITO!

Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’. NYUMA ya ukaribu wa Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, kuna siri nzito kufuatia mambo mbalimbali yanayojitokeza kati yao kila kukicha, Amani lina cha kukujuza. Katika kuunga maelezo hayo, inasemekana kwamba mbali na mambo mengine, hivi karibuni Diamond alimpelekea JK tuzo zake tano za kimataifa alizotwaa mwaka 2014 kwa kuwa nyuma yake kulikuwa na sapoti kubwa ya mkuu huyo wa nchi. UKARIBU MKUBWAKwa mujibu wa chanzo cha karibu ambacho ni ‘mtu’ wa Diamond, staa huyo amekuwa ‘klozdi’ sana na JK kufuatia mambo yake mengi ya msingi kuyafanya kwa kumshirikisha, kiasi kwamba kuna wakati Diamond hata akikurupuka usiku wa manane kama ana jambo huwa hasiti kumpigia simu mheshimiwa na kuongea kwa muda huku wakicheka weee! IKULU Habari hizo zilidai kwamba hata kama Diamond akishindwa kuzungumza naye kwa simu, kukicha mguu na njia hadi ikulu na kuzama ndani kama nyumbani kwao vile ambapo JK akiambiwa anasema ‘mwacheni aingie kijana wangu atakuwa na shida huyo’.
Source-GPL

No comments: