Wote tunapenda headlines nzuri kwenye
bongofleva ndio maana inapotokea kutokuelewana miongoni mwa watu wetu
tunaowakubali zitafanywa jitihada tu ilimradi tuyamalize kwa amani.
Baada ya Leo Tena ya CloudsFM kuwakutanisha Matonya na Tunda Man na kuyamaliza, Amplifaya ya CloudsFM pia March 27 2015 ilifanikiwa kubeba pande zote mbili za Nahreel na Quick Rocka ambao hawapatani.
Nahreel alikubali kuendelea kuusambaza upendo ambapo alianza kwa kusema >>> ‘Kiukweli
nilikua sielewani na Quick na hii ni baada ya yeye kusema niliondoka
kwenye studio yake Kiswahili yani bila kumuaga, huenda ni kweli
niliondoka hivyo lakini Quick hakuniajiri mimi, nilikwenda kumsaidia
kama msela wangu na kazi tulikua tunafanya kishkaji’
![]() |
NAHREEL |
‘Nilikua na
mipango yangu ya kufungua studio na nikafungua lakini pengine labda
jamaa hakufurahia mimi kuondoka pale, natafuta jinsi ya kukaa nae na
kuongea kama binadamu ili tuweke haya mambo sawa, nina mpango wa kwenda
kuongea tuyamalize’ – Nahreel.
Baada ya maneno ya Nahreel Quick akazungumza yafuatayo >>> ‘Hatukua
na mkataba wa maandishi bali wa maneno ndio maana nikatangaza kwamba
Nahreel sasa hivi yuko Switch, na alivyoondoka bila taarifa kibiashara
na mimi ilinikasirisha, kama yuko tayari kuyamaliza mimi niko poa… kama
anajua kweli alikosea na sasa anataka amani mimi sina tatizo’
![]() |
QUICK ROCKA |
Kama ulikua hujui, wakati huuhuu wa kutoelewana kwao Quick na Nahreel waliwahi kukutana Club, unataka kujua ilikuaje? bonyeza play hapa chini kusikiliza.
No comments:
Post a Comment