 |
| Vicent Kigosi"Ray" & Jacob Steven"Jb" |
Kuelekea mpambano wa watani wa jadi katika mchezo wa
mpira wa miguu hapa nchini, mchezo kati ya Simba na Yanga ambao
utafanyika hapo kesho kwenye uwanja wa taifa jiji Dar, Staa wa Bongo
Movies, Jacob Stephen ‘JB’ ambae ni mshabiki “kindakindaki” wa timu ya
Simba amemtaka Staa mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’ ambae ni shabiki wa
Yanga, aweke dau shilingi milioni moja kama alivyofanya mchezo uliopita
na yeye JB ataweka milioni mbili, kama Yanga ikishinda Ray atachukua
mzigo na kama Simba ikishinda JB atachukua mzigo huo.
“Weka milion, mimi naweka mbili sheria zinasema mwenye uhakika wa
ushindi ana point chache.si haki tukiweka sawa..si unakumbuka mara ya
mwisho tulipokutana.jaribu tena urudishe hela yako...”-JB aliandika na
kumtag Ray mara baada ya kuweka picha hiyo wakiwa pamoja.
No comments:
Post a Comment