Kwenye Bongo Fleva ishu ya Tunda Man na
Matonya kutokuwa na maelewano mazuri ni moja ya News zilizosikika sana, kila
mmoja alikuwa akilalamika tofauti kuhusu mwenzake, jana March 6 mastaa
hao walikutana kwa pamoja ndani ya studio za Clouds FM, wakati wa show
ya Leo Tena.
Tunda Man amesema anachohisi alimkosea Matonya
ni kusema kwamba alimtungia nyimbo lakini hataki tena kuzungumzia ishu
hiyo, amesema leo itakuwa mara ya mwisho kuzungumzia jambo hilo na
kuomba radhi kwa yote yaliyotokea, hana tatizo lolote na Matonya.
Matonya amesema kuwa Tunda Man
ni mdogo wake ambaye wamekutana vizuri na walikuwa wanaishi vizuri
lakini alipata wasiwasi baada ya kuona kila siku kuna maneno yanaibuka
ambayo hakupendezwa nayo, yeye binafsi anampenda Tunda Man na hata familia yake, kwa nafasi yake kama kaka ameamua kumsamehe.
Tunda amesema hawakuwahi kuonana tangu
mwaka 2007.. Matonya akamalizia kwamba kwa sasa wako tayari kwa pamoja
kuingia studio kufanya collabo.
Kusikiliza story yote ya Hekaheka bonyeza play hapa chini…


No comments:
Post a Comment