Wednesday, 4 March 2015

PAM D: SIMTEGEMEI MESEN KWENYE MUZIKI

Pam Daffa.
LEO tunaye mwanadada mtangazaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa ‘Pam D’ ambapo ameweka wazi kuwa mbali na undugu alionao na Mesen Selekta kila mtu anafanya kazi kivyake yaani yeye ni muandishi wa mistari, Mesen ni prodyuza na mwanamuziki. Akihojiwa na safu hii, huku akirekodiwa na ‘kruu’ ya Global TV Online mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chumba cha Habari cha Global Publishers, Pam D alisema mbali na kuwa muimbaji na mtangazaji yeye ni muigizaji na densa, ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia unaweza kuyapata kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com ; Pamela Daffa ‘Pam D’. Mwandishi: Ni lini kipaji chako cha kuimba kilianza kuonekana?
 Pam D: Kama kuanza sijaanza leo lakini rasmi nimeanza mwaka jana na ngoma yangu ya Nimempata ambayo nimeshirikiana na Mesen Selekta.
Mwandishi: Kwa mara ya kwanza kabisa wewe kuanza kuimba ulianza na wimbo upi?
Pam D: Niliimba wimbo ambao nilikuwa nimeshirikiana na Darasa kupitia Studio za Classic Sound chini ya Mona Gangstar lakini kipindi chote hicho sikuwa siriazi na wala sikujua watu wananichukuliaje lakini sasa hivi nimekuja rasmi.
Mwandishi: Wengi wanasema kwamba Mesen anakuinua sana kwenye muziki wako kuanzia kwenye utunzi wa mistari mpaka kukuandalia, ikoje hiyo?
Pam D: Ifahamike tu kwamba hata kama Mesen ni ndugu yangu lakini familia yetu sisi karibu wote ni wanamuziki na kwenye kazi kila mtu anafanya yake, mimi naandika mwenyewe na yeye ni prodyuza.

No comments: