Kifo cha msanii wa muziki AK47 wa nchini Uganda, kimeendelea kuzua
maswali hasa kutokana na taarifa mpya kuibuka kuwa, baunsa aliyeibuka na
kuandika maelezo polisi kuhusiana na namna alivyomkuta marehemu baada
ya kuanguka na kuzimia, siyo mwenyewe.
Taarifa
hizo mpya zimetolewa na mhudumu aliyekuwa eneo la tukio siku ya kifo
cha marehemu, taarifa ambazo zinaongezewa nguvu na ripoti ya msanii
Diamond Oscar aliyekuwa na marehemu siku ya tukio kuwa, waliletewa
taarifa ya kuanguka na kuzimia kwa marehemu na baunsa ambaye
hawamfahamu.
Sambamba na hisia kuwa huenda marehemu alishambuliwa na kuumizwa kabla ya kufariki, imefahamika kuwa Jumamosi iliyopita, marehemu aliingia katika ugomvi na mabaunsa katika baa nyingine iliyopo maeneo ya Cemetery Park huko Uganda.

No comments:
Post a Comment