Thursday, 5 March 2015

.WASTARA ASHEREHEKEA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA MWANAWE AKIMKUMBUKA SAJUKI.


Wastara,mtoto wake Farheen na aliyekuwa mumewe muigizaji Sajuki.
Katika hali iliyoonyesha kuwa bado anamkumbuka aliyekuwa mumewe aliyetangulia mbele ya haki,muigizaji wa kike nchini Wastara Juma ameonyesha hilo leo kupitia ukurasa wake wa Facebook alipokuwa akishiriki furaha ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mwanae,kwa kuandika maneno yanayoashiria kumkumbuka mzazi mwenzie huyo,hasa kwa siku hii anayofurahia kumbukumbu ya kuzaliwa binti yake huyu {Farheen},
Katika hili Wastara alikuwa na haya....... 
"Ulizaliwa ili wazazi wako furaha iongezeke na ukapewa jina la FARHEEN maana yake kufurahi furaha furahieni nasi tukafurahi ulizidisha furaha pale ulipotoka na sura copy ya baba yako SAJUKI kitu ambacho ni kumbukumbu yangu milele nitakulinda na kukupenda milele kwa uwezo wa ALLAH,"
Happy birthday my toto.....

No comments: