![]() |
| Charles Hilary mwenye Shati la Kitenge akitambulishwa rasmi "Azam Tv" |
MTANGAZAJI
mahiri nchini Charles Hillary aliyekuwa Shirika la Habari la BBC
jijini London leo ametua rasmi katika kituo cha Television cha
Azam TV kuungana na watangazaji wenzake.
Katika
tasnia ya habari, Charles Hillary amefanya kazi ya utangazaji
kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1993 akiwa Radio Tanzania Dar es
Salaam.
Mwaka 1994 alijiunga na Radio One ikiwa ni radio ya kwanza binafsi kuanzishwa nchini Tanzania.
Mwaka 1994 alijiunga na Radio One ikiwa ni radio ya kwanza binafsi kuanzishwa nchini Tanzania.
Mwaka
2003 aliamua kuacha kazi Radio One na kujiunga na Radio DW
Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani ambapo alifanya kazi mjini Koln
na baadaye Bonn hadi mwaka 2006 alipokatiza mkataba wake baada
ya kupata ajira Idhaa ya Kiswahili ya BBC London ambako
alijiunga tarehe Aprili 14, 2006.

No comments:
Post a Comment