Wednesday, 15 April 2015

Morogoro: Watu 10 wakamatwa Msikitini wakiwa na vifaa vya mlipuko

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NA POLISI.
Watu 9 wamekamatwa wakiwa wamejifungia kwenye msikiti wa Soni Morogoro wakiwa na vifaa vya milipuko hatari! Watu hao ni watanzania"!!

Katika purukushani hizo polisi mmoja amenusurika kuuawa baada ya kukatwa na jambia shingoni.

 Watu 10 wakamatwa ‪msikitini‬ wakiwa na milipuko, sare za jeshi, 'bendera ya Al Shabaab'

Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.

Katika tukio hilo, mmoja anayesadikiwa kuhusiana na watu hao waliokamatwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumjeruhi kwa panga askari polisi aliyekuwa akipambana naye.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14 mwaka huu) majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.

 
BAADHI YA VITU VILIVYOKAMATWA.

No comments: