Sunday, 31 May 2015

ALICHOKIONGEA Mh WASSIRA WAKATI AKITANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA URAIS 2015

TANGU MMENIJUA HAMJAWAHI SIKIA NINA KASHFA YA RUSHWA - WASSIRA



Wassira: Leo nimekuja hapa Mwanza kwaajili ya kukata ukimya na kutangaza rasmi nia ya kugombea Urais wa Tanzania 2015. #WassiraUrais2015

Wassira: Sababu za mimi kugombea Urais, kwanza ni haki yangu ya msingi, pili naijua vizuri Tanzania.

Wassira: Mimi ni miongoni mwa Watanzania wachache wanaoijua vizuri Tanzania ya jana, ya leo na Tanzania ya kesho.

Wassira: Baada ya kutafakari kwa muda nimeamua kugombea nafasi hii ya juu maana nimeona ni wakati sahihi kwangu.

Wassira: Mambo ya msingi nitayozingatia kwenye uongozi wangu ni kuendeleza Tanzania imara, umoja, amani na mshikamano.

Wassira: Nitahakikisha Mahakama, Serikali na Bunge zinaimarishwa.

Wassira: Nitasimamia utumishi wa umma uimarishwe zaidi na kuhakikisha unatoa shughuli zake kwa usahihi

Wassira: Serikali yangu itahakikisha uchumi wetu unaendelea kukua juu zaidi na Watanzania kuwezeshwa na kuendesha uchumi

Wassira: Ajira kubwa itakayoweza kuwakomboa vijana ni kuwezesha vijana kuwa wabunifu ili kuweza kujiajiri wenyewe.

Wassira: Pia ninaamini sekta kubwa itakayowezesha ajira kwa vijana ni kilimo, muhimu ni kuwa na vifaa vya kisasa.

Wassira: Pia ni kuboresha elimu yetu ili iwe ya kisasa zaidi na wasomi wetu waweze kupambana na soko la Afrika na Dunia.

Wassira: Suala la afya ikiwezekana tutahakikisha kila Mtanzania anakuwa na bima ya afya kumuwezesha kupata matibabu.

Wassira: Kuna watu wanalalamika tu kuhusu barabara, waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Wassira: Nchi yetu ina tatizo kubwa la rushwa, ukikataa hili lazima kesho litakuumbua, unapozungumza hili itoke moyoni

Wassira: Hata serikali ya kijiji leo rushwa imetawala,unapoenda kuomba barua unaambiwa njoo kesho lengo lake umpe rushwa.

Wassira: Tangu mmenijua hamjawahi kusikia nina kashfa ya rushwa, ilipotajwa kashfa ya EPA na ESCROW zote sijahusishwa

Wassira: Ikulu hamuwezi kuweka mla rushwa maana mkiweka mla rushwa pale siku nyingine atauza IKULU yenu

Wassira: Muajiriwa huwezi kuwa Tajiri maana mshahara wako ni Kula na uishe,ukiona muajiriwa Tajiri jiulize ameupata wapi

Wassira: Tutawekeza katika usalama na jeshi letu litakuwa dogo ila tutahakisha linakuwa bora na imara lenye nguvu.

Mh Stephen Wassira amemaliza kuongea sasa baada ya kutangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais wa Tanzania 2015.

NB:-FUATILIA KWA SEHEMU VIDEO YA HOTUBA YAKE HAPO CHINI,
HABARI - TBC | MAY.31.2015

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushrika Mhe. Steven Wasira ametangaza nia yake ya kuwania Urais huku akiahidi kumaliza rushwa.

Posted by Simu.TV on Sunday, May 31, 2015

No comments: