Siyo picha ya kwanza kutoka ikimuonesha Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akiwa
amesinzia kwenye matukio mbalimbali makubwa.. safari hii Mzee Mugabe amepigwa tena
picha akiwa amesinzia wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.
Waziri wa Mawasiliano Zimbabwe, Prof. Jonathan Moyo ameingia kwenye ukurasa wake wa @Twitter na kupost Tweets zikionyesha kuchukizwa na kitendo cha waandishi nchini Nigeria kumuanika rais huyo kwa picha walizompiga akiwa amesinzia kama inavyoonekana hapo juu !!
Sahara Reporters wanalaumiwa moja kwa moja kwa kupiga picha hiyo na kuisambaza mitandaoni.
Hapa nina picha za viongozi ambao waliwahi kupigwa baada ya kukutwa wamesinzia.
![]() |
| Abdurrahman Wahid, picha hii ilipigwa wakati huo alikuwa Rais wa Indonesia |
![]() |
| Naoto Kan, aliwahi kuwa Waziri Mkuu Japan na Waziri wa Fedha vilevile |





No comments:
Post a Comment