![]() |
| Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dkt Jakaya.M.Kikwete. |
Kikao cha Usalama na Maadili cha CCM, kukutana leo saa nane mchana
Leo Kamati ya Maadili inakaa.
1. Kikwete
2. Mwinyi
3. Mkapa
4. Kinana
5. Mangula
6. Nape
7. Katibu wa Vijana Taifa
8. Mwenyekiti wa Vijana Taifa
9. Mwenyekiti wa Wazazi Taifa
10. Katibu wa Wazazi Taifa
11. Dr Shein
12. Mwenyekiti wa Wanawake Taifa
13. Katibu wa Wazazi Taifa
14. Msekwa
15. Malecela
16. Salum Ahamed Salum
17. Msuya
18. Mkuu TAKUKURU ( Mwalikwa)
19. Mkuu Usalama ( Mwalikwa).
Kikao cha Usalama na Maadili cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya
Mwenyekiti wake Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kinatarajia kuanza majira
ya saa nane mchana huu katika ukumbi wa NEC uliopo ofisi za Makao Makuu
ya CCM, mjini Dodoma maarufu kama Whitehouse.Kikao hicho chenye wajumbe 13 wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg Jakaya Kikwete, Makamu M/kiti wa CCM Ndg Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana kitajadili majina 38 ya makada wa CCM waliochukua fomu za kugombea nafasi ya Urais.
Kikao hiki ndicho kikao cha juu zaidi cha Maadili chenye uwezo wa kujadili juu ya Mwenendo, Tabia, Uadilifu na Rekodi za Kiutendaji na Nidhamu ya Kila mmoja katika wagombea wote 38.
Mwenyekiti
wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete atastaafu baada ya uchaguzi huo
akiwa amemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho madarakani, kwa mujibu
wa Katiba.
Maafisa wa ngazi ya juu wa chama hicho watawachagua wagombe watatu, ambao hatimae watapigiwa kura katika mkutano mkuu Julai12 kumpata mgombea Urais.
Miongoni mwa wanasiasa wanaotajwa zaidi ni Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal, Waziri mkuu Mizengo Pinda, Jaji mstaafu Agustino Ramadhani, Waziri wa mambo ya nchi za nje Benard Membe na Waziri mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Pia katika orodha ya wagombea 39 yumo waziri wa sheria aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

No comments:
Post a Comment