Monday, 13 July 2015

DIAMOND, PENNY USO KWA USO KWENYE AROBAINI YA MTOTO WA AUNTY EZEKIEL.

Peniel Mangilwa"Penny"
Ule usemi wa kwamba milima haikutani, binadamu hukutana umejidhihirisha baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kukutana uso kwa uso na aliyekuwa mchumba’ke, Penniel Mwigilwa ‘Penny’ kwenye shughuli ya 40 ya mtoto wa mwigizaji, Aunt Ezekiel hivyo kupata fursa ya kukumbushia enzi zao.
Diamond & Penny walivyokutana.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala, Dar ambapo pati hiyo ilihudhuriwa na mastaa kibao.
Katika tukio hilo, Diamond ndiye aliyeanza kumuona Penny akamwita kwa lengo la kumsalimia ambapo naye alitii akionekana mwenye furaha kisha walikumbatiana huku baadhi ya waalikwa wakiwataka kukumbushia enzi za mapenzi yao.
Pichani Diamond na Meneja wake"Babu Tale"wakipata Futari kwenye Arobaini ya Mtoto wa Aunt Ezekiel"Cookie"
Baada ya salamu, waliendelea kuzungumza ‘mambo yao’ huku muda wote wakicheka.
Baadaye, Penny aliwasalimia baadhi ya watu waliokuwa wamekaa na Diamond na kwenda kukaa pembeni yao huku akitazamana na Diamond kwa shauku kubwa.
Aunt Ezekiel alivyotokelezea siku ya Arobaini ya mwanae"Cookie".
  wawili hao walikaa pamoja kwa muda ambapo muda mwingi walikuwa wakitaniana huku Romy Jones akichagiza utani huo.Hata hivyo, baadaye Romy alinyanyuka alipokuwa ameketi na kwenda kwa Penny kama mtu aliyeagizwa jambo na Diamond ambapo walizungumza kwa kirefu.
Moze Iyobo,Aunt Ezekiel na Mtoto wao"Cookie"
Alipoulizwa Penny kulikoni yeye na Diamond kuwa gumzo mahali hapo, alisema kuwa hana sababu ya kununa maana hakuna kibaya ambacho kipo kati yake na jamaa huyo kwani wamekuwa wakiwasiliana na kuongea vizuri ingawa kila mtu ana mambo yake.
“Hapa tumealikwa na kila mtu amekuja kivyake, sasa si rahisi ukawaona watu usiwasalimie au uchukie maana hakuna sababu ya kufanya hivyo, sina ugomvi na Diamond na sina mipaka yoyote ya kusalimiana au kuongea naye,” alisema Penny.

 Kwa upande wa Diamond alisema kuwa alikuwa pale kwa ajili ya kufuturu na kumfurahia kila mtu hivyo hakuna dhambi yoyote kwake kusalimiana na Penny.
Source-GPL.

No comments: