Tuesday, 21 July 2015

LEMBELI AJIENGUA CCM.

Mbunge wa Kahama, James Lembeli
Mbunge wa Kahama, James Lembeli ametangaza rasmi kujiunga na CHADEMA. 
Lembeli ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar.

-Kwa muda mrefu Bw,James Lembeli amekuwa na mgogoro wa chinichini na Chama chake cha zamani{CCM}

 Mbunge wa Kahama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw,James David Lembeli (kushoto) akiingia ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mtoto wake, Wizilya Lembeli wakati akienda kutangaza rasmi kuondoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Mbunge wa Jimbo la Kahama Bw,James Lembeli (CCM), ametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Lembeli, ametangaza msimamo huo leo Julai 21, 2015 Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa, ameamua kuhama CCM kutokana ana sababu mbalimbali ikiwemo kukithiri kwa vitendo vya rushwa.
Hata hivyo, amesema kumekuwa na matukio mengi ya rushwa ikiwemo wana CCM kununuliwa kadi za chama na kupewa rushwa na watu wanaowania ubunge na kwamba licha ya kuripoti vitendo hivyo katika mamlaka husika hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
 Aidha, amefafanua kwamba mwaka 2010, aliwahi kudanganywa na viongozi wa CCM kuwa agombee ubunge katika Jimbo la Ushetu ambalo halikuwepo, jambo lililomuonyesha kutohitajika kwake na chama hicho. Mbunge huyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii, ametaja sababu nyingine ya kuhama CCM kuwa ni kutoridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM.
Ameweka bayana kwamba atagombea ubunge kupitia Jimbo la Kahama Mjini, kupitia CHADEMA, baada ya kuombwa na wananchi ambao amewaasa kuendelea kumpa ushirikiano licha ya Jimbo hilo kugawanywa na kuwa majimbo mawili.

No comments: