Leo Lowassa amezungumza kwenye kikao cha UKAWA Bahari Beach, Dar es salaam,ambapo viongozi mbalimbali wa UKAWA walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia hatma yake kuelekea Ikulu pamoja na upungufu uliojitokeza wakati wa uchaguzi wa kumpata mgombea Urais wa CCM.
Amesema baada ya kutafakari kwa kina na kujiridhisha ameamua kujiondoa CCM na kuitikia wito wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Amesema pia safari yake haitafanikiwa iwapo hawatajitokeza watu wengi kupiga kura, na anaiomba Tume ya uchaguzi NEC kuongeza muda wa kujiandikisha ili watu wote waweze kujiandikisha kama ilivyofanya katika Mikoa mbalimbali.
Pia amesema alinyimwa haki yake na CCM kama Mtanzania kujieleza na kujitetea, hivyo atakua mnafiki akisema ana imani na chama hicho.
NB:-MUANGALIE Mh,EDWARD NGOYAI LOWASSA AKITANGAZA RASMI KUACHANA NA CCM,NA KUJIBU BAADHI YA TUHUMA ZILIZOPELEKEA KUJIUZULU UWAZIRI MKUU.
MBIO ZA URAISI - JULY.28.2015 | AZAM TVMh. Edward Lowassa akana tuhuma za ufisadi wa RICHMOND, asema amechoshwa na kelele hizo hivyo mwenye ushahidi apelike mahakamani.
Posted by Simu.TV on Tuesday, July 28, 2015
MBIO ZA URAISI - JULY.28.2015 | AZAM TVMh. Lowassa ajibu maswali ya waandishi mbalimbali walio hudhuria mkutano huo huku akieleza masuala mbalimbali ikiwemo hofu ya kulipiza kisasi.
Posted by Simu.TV on Tuesday, July 28, 2015



No comments:
Post a Comment