Yule mwanaume aliyezaa na Staa wa Bongo Movies na
Bongo Fleva,Shilole,aitwaye Elias Makala ameibuka na kuzungumza na U heard ya Clouds Fm na
Soudy Brown juzi kuwa hakuwahi kumbaka msaniii huyo kama ambavyo anazungumza
kwenye vyombo vya habari.
‘’Mimi namshangaa sana Shilole anavyosema kuwa nilimbaka,sijawahi kumbaka nilikuwa naishi naye kama mume na mke kwa zaidi ya miaka saba, na nilimuuliza kwanini anasema uongo kuwa nilimbaka alinijibu kuwa habari hiyo inamsaidia kumpaisha (kick) kwenye muziki wake,’’alisema Makala.
Hata hivyo alipoulizwa kama anasikia wivu anaposikia na kumuona Shilole akila raha na mpenzi wake mpya msanii Nuh Mziwanda alisema kuwa haoni wivu kwa kuwa Nuh anakula makombo yake kwani yeye ndiye aliyeanza kuwa na msanii huyo.
‘’Sioni wivu kabisa miye ndiyo niliyeanza huyo Nuh anakula makombo yangu,hata hivyo mimi nina mke na familia yangu huku Igunga,’aliongeza Makala.
Msanii Shilole alipoulizwa alisema kuwa hawezi kumzungumzia mwanaume huyo ambaye hajui kama mtoto wake anaishi vipi,anasoma wapi, na anakula nini.
‘’Huwa sipendi kabisa kumzungumzia mwanaume huyo ambaye hajui mtoto wake anaishi vipi,anasoma wapi na anakula nini,’’alijibu Shilole.
Source-XXL{Clouds Fm}

No comments:
Post a Comment