Friday, 10 July 2015

WANANCHI WACHOMA MOTO KITUO CHA POLISI BUNJU-A LEO.

Wananchi wenye hasira kali wamechoma moto Kituo cha Polisi Bunju 'A' na Askari wote kukimbia, kwa ujumla hali haikuwa shwari kwa takriban lisaa lizima huku barabara ikifungwa.

Taarifa zinadai Mahabusu waliokuwa ndani ya Mahabusu iliyo kituoni hapo wametoka salama baada ya kufunguliwa na msamaria mwema.

 Tukio hilo limetokea baada ya mtoto mmoja wa shule kugongwa na gari,na kusababisha Watoto wa shule ya msingi kulala barabarani huku raia wakiwa wameshika mifagio na magongo makini kuangalia kinacho endea.


No comments: