Wednesday, 29 July 2015

Yaliyojiri kwenye Mkutano wa CCM Dar July 29 2015

Kupitia tangazo ambalo lililotolewa siku ya jana July 28 2015 mitandaoni ikiwa na taarifa  kuwa CCM watafanya Kikao chao Makao Makuu Madogo July 29 2015 Lumumba Dar siku ya leo.

Katika kikao hicho Katibu Mwenezi wa CCM Dar, Juma Simba Gaddafi ndio Kiongozi pekee wa CCM aliyefika kwenye Mkutano huo ambao umefanyika Peacock Hotel Dar, na hii ni sehemu ya alichokisema.
CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru‘>>>
Kwenye sentensi nyingine amesema hivi >>> ‘Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda‘>>>
Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri… Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika‘>>>
Hiki ndio alichokijibu kuhusu ishu ya Lowassa kuhamia CHADEMA >>> ‘Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka‘>>>
Haya ni majibu yake mengine kuhusu Lowassa kutoka CCM >>> ‘Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara‘ >>>> Juma Simba Gaddafi.

FUATILIA VIDEO ZA TUKIO ZIMA HAPA:-
MBIO ZA URAISI - JULY.29.2015 | AZAM TV

Waandishi wa habari wahoji tuhuma za Lowassa kuenguliwa na Mkutano mkuu huku wakitaka udadavuzi kuhusu mgawanyo wa majukumu kati ya tume ya maadili na usalama.

Posted by Simu.TV on Wednesday, July 29, 2015
MBIO ZA URAISI - JULY.29.2015 | AZAM TV

CCM Wasema hawana hofu juu ya sakata la Lowassa kuhamia Chadema na kusema wanaamini watashinda kwa kishindo kikubwa.

Posted by Simu.TV on Wednesday, July 29, 2015
MBIO ZA URAISI - JULY.29.2015 | AZAM TV

Katibu mwenezi wa CCM Juma Simba asema hawana muda wa kuzungumzia suala la Lowassa ni bora kuongelea suala la BVR linatija kwao.

Posted by Simu.TV on Wednesday, July 29, 2015
MBIO ZA URAISI - JULY.29.2015 | AZAM TV

Waandishi wa habari wasema CCM walipaswa kuzungumzia masuala mazito yaliyojili Nchini na sio kwaajiri ya kuwashukuru waandishi.

Posted by Simu.TV on Wednesday, July 29, 2015
MBIO ZA URAISI - JULY.29.2015 | AZAM TV

Katibu mwenezi Juma Simba asema watashida kwa kishindo kwani uwepo wa Jembe Magufuli kutawafanya watambe ifikapo Oktoba.

Posted by Simu.TV on Wednesday, July 29, 2015

No comments: